Saturday, December 03, 2011

UTABIRINYANYA NI PUMBA AU NI SILAHA?



Baada ya ngono, sidhani yapo mambo yaliechapishwa mtandaoni (World Wide Web) kuliko Utabirinyanya (biorhythms).

Pamoja na kuwa utabiri huu unao mamilioni ya wafuasi duniani kote, wengi katika wataalam nawasomi wanasema mambo hayo ni "pumba" kabisa.


Mimi binafsi, nikiwa mmoja katika wafuasi wa aina hii ya utabiri, nia yangu katika blogu mpya hii ni kukufanyia nawe utabiri kama ninavyojifanyia mimi mwenyewe.


Kwa madhumuni yakuuliza kwa undani, labda uniandikie na nitakujibu hadharani au kisiri unavyopenda wewe kwamba je dunia hii yatumiaje "ujuzi" wa utabirinyanya, yatosha nikuambie misingi yake.


Unaambiwa siku yako ya kuzaliwa ulipewa siku 11 zakwanza ukiwa na nguvu za kutosha mwilini mwako: uliweza kulia kwa sauti kubwa zaidi, kupiga chafya ya kibogo, kurusharusha mikono na vijimguu vyako kwa nguvu ya kumshangaza kweli hata mama yako mzazi

Lakini, siku 12 ziliofuata ukawa UMETULIA kidogo  hata kiasi cha kuwa mdhaifu kidogo... nguvu na makelel ya kuzidi vikapunguga wastani.


Mwisho wa hizo siku mbili ukaanza tena UPYAAAA!!! Ukarudia zile siku 11 zanguvu za pale mwanzoni ....na kadhalika na kadhalika na hayo ndiyo maisha yako hadi leo hadi kaburini pia  11    12     11     12    11    12    11    12....

Hivyo hivyo (mutatis mutandis) ukapewa pia siku za kwanza 16 ukiwa akili yako inafanya kazi vizuri kwa kuamua mambo, halafu siku 17 zenye udhaifu katika ngazi za kimawazo. 16    17    16    17    16    17    16    17    16    17....

Hizo zote kama mifano ya hapo juu zinaitwa mizunguko ya utabirinyanya (BIORHYTHMIC CYCLES).  Nayo mizunguko hii ni zaidi ya nilivyotaja (soma tu popote pale mtandaoni ili upate mizunguko mingine na kujifanyia wewe mwenyewe mahesabu ya hali yako ilivyo leo au atakavyokua katika siku fulani au mtihani fulani ujao).

Yatosha kwangu kukuambia hayo mahesabu mimi nimekwisha kufanyia kama tutakuwa wote katika blogu hii, na kama wewe binafsi hujatoshelezwa kuwa huru kuniuliza ili nikusaidie zaidi.

La pili na la muhimu kiliko yote, elewa kwamba utabiri huu sio BADALA ya kuwaona wataalam kama unamatatizo ya kimaisha au kiafya.  Watu kama madaktari na wa ustawi wa jamii ndizo kazi zao kuwasaidia watu wenye hali ya mfadhaiko na madhara kama hayo, usije ukategemea hata siku moja utabiri wangu pamoja na kwamba na amini kabisa utabiri huu ni silaha nzuri kutumia katika vita vya maisha!

No comments:

Post a Comment